Marekani-Sheria

Troy Davis anyongwa licha ya rufaa nyingi kutolewa

RFI

Licha ya juhudi za uhamasishaji, hakuna muujiza wowote uliotokea ambao ungelisbabisha Troy Davis kutonyongwa. Mmarekani huyo mweusi aliuawa kwa kudungwa sindano Jumatano saa tano na dakika 8 usiku majira ya Marekani sawa na saa kumi na moja na dakika 8 asubuhi alhamisi majira ya Paris. Amefahamisha hayo mlinzi wa jela la Jackson katika jimbo la Georgia.

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kunyongwa kwake, Mmarekani huyo mweusi mwenye umri wa miaka 42 mara kwa mara alisisitiza kuwa hana hatia yeyote kuhusu kifo cha askari polisi mzungu ambapo aliwekwa mbaroni tangu mwaka 1991.

Haikuwa kosa langu, sikuwa na silaha, alisema hayo Troy Davis. Kwa mujibu wa muandishi wa habari alieshuhudia pamoja na wazazi wake kunyongwa kwa mtuhumiwa huyo.

Kabla ya kuonyongwa Troy aliwaambia waliokuwa tayari kutekeleza kitendo hicho “Mungu awabariki”. Mamia kadhaa ya waandamanaji walikusanyika Karibu na gerezani la Jackson, wakiwa na matumaini kwamba hukumu hiyo haitatekelezwa.

REUTERS

Waandamanaji hao waliimba "Tafadhali usiruhusu kifo cha Troy Davis 'na' Mimi ni Troy Davis!" Maandamano, ambayo yalianza mapema mchana, chini ya ulinzi mkali wa polisi hku watu 2 wakitiwa nguvuni.

Tukio hilo la kunyongwa kwa Troy lilipangwa kufanyika saa moja jioni, lakini lilicheleweshwa kwa zaidi ya saa nne, ukisubiriwai uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani, ambayo hatimaye iliruhusu mauaji.

Kifo cha Troy Davis kilikamlika dakika kumi na tano baada ya utekelezaji. Mamia ya waandamanaji waliokuwa nje ya gereza walihuzunika kupokea habari hiyo ya kifo cha Troy baada ya kusalia muda mrefu wakiwa na matumaini ya uwezsekano wa mahakama inasitisha tukio hilo.

Picha ya Troy Davis,
Picha ya Troy Davis, REUTERS/Tami Chappell

Serikali ya Ufaransa kupitia katika taarifa ya Wizara ya mambo ya nje, imesema kusikitishwa na hatuwa hiyo ambayo imechukuliwa licha ya rufaa nyingi kutolewa kwa ajili ya msamaha.