Palestina-France

Wapalestina wakaribisha mpango uliopendekezwa na Ufaransa

Mkutano wa UN
Mkutano wa UN RFI

Wapalestina kuwakaribisha mpango wa rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kwa ajili ya Mashariki ya Kati. Nicolas Sarkozy amependekeza hadhi ya Wapalestina katika Umoja wa Mataifa, kuwa kama taifa angalizi kwenye baraza hilo kama jinsi ilivyo Vatican na kuanza kwa mazungumzo na Israeli kabla ya mkataba wa amani katika mwaka mmoja. Upande wake, Barack Obama, asema hakuna taifa la Palestina bila ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Israeli na Wapalestina. Hiyo ndio iliokuwa hoja yake wakati wa mkutano wake na Mahmoud Abbas katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.  

Matangazo ya kibiashara

Mpango uliowasilishwa na Nicolas Sarkozy unaweza kuwa njia ya kutanzua mgogoro kwa ajili ya Wapalestina. Bila shaka, Mahmoud Abbas atawasilisha Septemba 23, 2011 ombi lake kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kama alivyopanga kuomba uanacahama wa Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo mbunge Hanani Ashraoui amesema kuna uwezekano kwa Wapalestina kukubali hadhi ya kati kwa nchi zisizokuwa wanachama, kama ilivyopendekezwa na Ufaransa.

Kiongozi huyo amesema "Wakati tulijadiliana na rais, tuliona ni wazo chanya. Ni fikra nzuri ambayo inaweza kuingiza utashi wa kisiasa na katika kile sisi tunaona kama ni jitihada za Wamarekani kudhoofisha Wapalestina."

Kupitishwa kwa azimio katika Mkutano Mkuu, itakuwa ishara ya ushindi kwa Wapalestina. Nicolas Sarkozy amependekeza azimio hilo lifutishwe na kuanza kwa mazungumzo, na ratiba ili rasmi: miezi sita kufikia makubaliano kuhusu mipaka na usalama, mwaka mmoja kwa makubaliano ya jumla.

Israeli imekaribisha pendekezo hilo la Ufaransa kwa baridi sana , ambapo Benjamin Netanyahu amesema wamekubali.