Palestina-UN

Licha ya vitisho vya Marekani Mahamoud Abbas atawasilisha ombi lake UN

RFI

Pamoja na kuwepo kwa vitisho vya Marekani kutumia kura yake ya veto, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anajiandaa kuwasilisha hoja ya kuomba uanachama ndani ya Umoja wa Mataifa. Mahmoud Abbas atawasilisha ombi lake kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na baadae atahutubia kikao cha Umoja wa Mataifa ambapo hutba yake itapeperushwa moja kwa moja na vituo mbalimbali na kuonyeshwa wananchi wa Palestina

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa mamlaka ya wa Palestina atahutubia kikao cha Umoja wa Mataifa Ijumaa hii Septermba 23, saa tisa na dakika 35 majira ya Ufaransa  ambae atafuatiwa baadae na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyau.

Ukweli ni kwamba wa Palestina wamefaanikisha kuzungumzwa sana mwaka huu kwenye Umoja wa Mataifa. Viongozi was mataifa mbalimbali wamekuwa wakigusia swala la mzozo wa Palestina na kujaribu kuepusha mgongano wowote ambao waweza kutokea.

Marekani Imekuwa katika harakati za kuhakikisha kuwa Abbas anabadili mpango huo juhudi ambazo hata hivyo zimegonga ukuta.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema kwa vyovyote vile wanasubiri kitachotokea baadae. waziri huyo amesema hivbyo kwa sababu anafahamu fika kwamba iwapo Abbas atawasilishwa ombi lake hilo kura haitapigwa papo hapo, itachukuwa wiki kadhaa

Kura ya Turufu

Hadi kufikia hatuwa hiyo inaweza kuchukuwa wiki kadhaa. Ufaransa itatumia muda huo kuhakikisha kura hiyo ya turufu ya marekani haitekelezwi na kuepuka maadamano ya huku na kule katika nchi za kiarabu. Hata hivyo bila mbali na kura ya turufu, ili ombi hilo la Palsetine liweze kupasishwa lazima liungwe mkono na nchi 9 kati ya 15 zinazo unda baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa.

Hadi sasa  wajumbe 5 wanaunga mkono ombi la Palestina ikiwa ni pamoja na Chine,  Russie, Brasil, Liban na Afrika Kusini ambazo zinataka Palestina iwe mwanachama wa kudumu katika baraza la Umoja wa Mataifa.

Marekani inapinga vikali mpango wa Palestina. Colombia ambayo pia ni mwanachama wa baraza la Usalama la UN itakata kuonyesha msimamo wake. Hali ambayo inawapa nguvu wa Marekani. Ujumbe wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa wamethibitisha kuwa  Bosnie, Gabon na Nigéria wanatiwa tumbo moto ili wapinge ombi la Palestina.