Zimbabwe-UN

Rais Mugabe aishutumu ICC kufumbia macho uhali wa viongozi wa nchi za magharibi

RFI

Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe ameshutumu mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC kupuuza vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na viongozi wa nchi za Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Mugabe ameuambia mkutno wa Umoja wa Mataifa kuwa ICC haiaminiki Barani Afrika kwa kuwa imekuwa ikijihusisha na viongozi wa nchi zinazoendelea pekee wengi wao Waafrika.

 

Mugabe amesema viongozi wa mataifa yenye nguvu wamekuwa wakifanya uhalifu wa kimataifa akitolea mfano viongozi wa zamani, wa Marekanai George W Bush na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tonny Blair.

Mugabe pia ametupa lawama zake kwa majeshi ya kujihami NATO kufanya mashambulizi ya Anga kwa kisingizio cha kulinda raia