Marekani

IMF yaonya kuhusu madeni, Benki ya Dunia kusaidia Pembe ya Afrika

Reuters/Shannon Stapleton

Shirika la Fedha Duniani, IMF limetoa onyo ya kwamba halitakuwa na fedha za kutosha kuweza kutoa mkopo kwa mataifa zaidi ya Barani Ulaya iwapo tatizo la madeni litaendelea kuongezeka kwenye mataifa zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Christine Lagarde amesema dunia inahaha katika kuhakikisha inakabiliana na matatizo yaliyopo lakini iwapo kutakuwa na ongezeko la mgogoro huo basi hali itakuwa mbaya zaidi.
Hatua hii inakuja wakati huu ambapo Masoko ya Hisa yakiendelea kupanda na kushuka na kuzua hofu huenda hali ikazidi kuwa mbaya katika mataifa mengi yanayofanya biashara hiyo.
Wakati huohuo Benki ya Dunia imetangaza mpango wake wa kuongeza fungu zaidi kwa ajili ya kukabiliana na hali ya ukame ambayo inatikisi eneo la Pembe ya Afrika na sasa itatoa takribani dola bilioni mbili kusaidia waathirika.
Benki ya Dunia imesema fedha hizo zitatumika katika kuhakikisha inaimaridha huduma za kibinadamu ambazo zinahitajika kwa sasa nchini humo pamoja na kukabiliana na utapiamlo ambao umewakumba watoto wengi.
Licha ya kutolewa kwa fedha hizo na Benki ya Dunia lakini imekiri kuwa fedha zaidi zinahitajika katika kuhakikisha chakula cha uhakika kinapatikana kwa wananchi zaidi ya milioni kumi na tatu waliokumbwa na janga hilo.IMF yaonya kuhusu madeni, Benki ya Dunia kusaidia Pembe ya Afrika
Shirika la Fedha Duniani, IMF limetoa onyo ya kwamba halitakuwa na fedha za kutosha kuweza kutoa mkopo kwa mataifa zaidi ya Barani Ulaya iwapo tatizo la madeni litaendelea kuongezeka kwenye mataifa zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Christine Lagarde amesema dunia inahaha katika kuhakikisha inakabiliana na matatizo yaliyopo lakini iwapo kutakuwa na ongezeko la mgogoro huo basi hali itakuwa mbaya zaidi.
Hatua hii inakuja wakati huu ambapo Masoko ya Hisa yakiendelea kupanda na kushuka na kuzua hofu huenda hali ikazidi kuwa mbaya katika mataifa mengi yanayofanya biashara hiyo.
Wakati huohuo Benki ya Dunia imetangaza mpango wake wa kuongeza fungu zaidi kwa ajili ya kukabiliana na hali ya ukame ambayo inatikisi eneo la Pembe ya Afrika na sasa itatoa takribani dola bilioni mbili kusaidia waathirika.
Benki ya Dunia imesema fedha hizo zitatumika katika kuhakikisha inaimaridha huduma za kibinadamu ambazo zinahitajika kwa sasa nchini humo pamoja na kukabiliana na utapiamlo ambao umewakumba watoto wengi.
Licha ya kutolewa kwa fedha hizo na Benki ya Dunia lakini imekiri kuwa fedha zaidi zinahitajika katika kuhakikisha chakula cha uhakika kinapatikana kwa wananchi zaidi ya milioni kumi na tatu waliokumbwa na janga hilo.