Libya

Mapambano makali yaendelea katika mji wa Sirte nchini Libya

Wapiganaji wa NTC
Wapiganaji wa NTC Reuters

Ikiwa ni siku ya tatu ya mfululizo wa mapambano makali katika mji wa sirte nchini Libya, wapiganaji wa baraza la mpito la NTC wasema wamefaanikiwa kuingia katika baadhi ya maeneo ya mji huo kutokea mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Moshi wa mabomu umeendelea kutanda katika anga ya mji wa Sirte ambako ndege za NATO kwa kushurikiana na wapiganaji wa NTC wameendelea kushambulia ngome zinazoshikiliwa na wapiganaji wanaomuunga mkono kanali gaddafi.

Wakati mapigano hayo yakiendelea hofu ya usala wa raia waliobakia katika mji huo imeendelea kuwa ya wasiwasi kufuatia wale waliofanikiwa kutoroka kwenye mji huo kudai kuwa hawafahamu lolote endapo mji wa Tripoli uko chini ya waasi.

Majeshi ya NATO yameshindwa kuendelea na mashambulizi zaidi ya anga kufuatia wapiganaji wa kanali gaddafi kuwatumia raia kama Ngao.