Palestina

Marekani na Ulaya walaani vikali mpango wa Israeli wa kujenga makazi zaidi mashariki mwa Jerusalem

Ukuta wa Gaza
Ukuta wa Gaza Ahmad/Gharabli/AFP

Ulaya na Marekani wamelaani vikali mpango wa Israeli wa kujenga makazi zaidi ya elfu moja na mia moja katika eneo la Mashariki mwa Jerusalem kitu kilichowafanya Palestina kusema mazungumzo ya upatanishi hayawezi kufanikiwa.

Matangazo ya kibiashara

Marekani licha ya kuweka bayana nia yao ya kupiga kura ya turufu kupinga Palestina kupewa uanachama wa Umoja wa Mataifa UN imeonekana kutokuwa tayari kushuhudia ujenzi huo ukitekelezwa kwa sasa.

Marekani, Ulaya na Umoja wa Mataifa UN umeshawishika kusema iwapo hatua hiyo ya ujenzi itatekelezwa basi hakutakuwa na mazungumzo ya kupata suluhu ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mataifa hayo ya Ulaya na Marekani yanaonya kwamba utekelezwaji wa hatuwa hiyo Mashariki mwa mji wa Jerusalem, huenda likawa kikwazo cha amani kati ya Israel na Palestina.

Ujenzi huo uliotanagzwa na wizara ya ndani ya Isreal,unatazamiwa kufanyika katika eneo la hilo.

Palestina imeomba kutambuliwa kama taifa la kujitegemea katika baraza la Umoja wa Mataifa, na ombi lao sasa linasubiriwa kupigiwa kura katika baraza la usalama la umoja wa mataifa,huku Marekani ikisema kuwa itatumia kurayake ya turufu kuinga hatua hiyo ya Palestina.