Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kufikia muafaka juu ya vikwazo kwa Syria

Kikao cha baraza la uslama UN
Kikao cha baraza la uslama UN RFI

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa hapo jana limemaliza mazungumzo yake juu ya nchi ya Syria bila kufikia mwafaka juu ya kuja na maazimio mapya baada ya Urusi kufifisha juhudi za Ulaya kutishia kuiwekea vikwazo Syria.

Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo lilijadili mapendekezo ya maazimio juu ya machafuko ya nchini Syria yaliyowasilishwa na Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Ureno huku Urusi ikipinga hatua hiyo.

Nchi hizo zilipendekeza maazimio mapya ya vitisho kwa rais wa Syria Bashar Al Assad kumchukulia hatua ikiwa atakaidi amri ya kuacha kuwashambulia Raia wake.

Akieleza kutoafiki mapendekezo hayo Balozi wa urusi ndani ya umoja wa mataifa,Vitaly Churkin amesema mapendekezo hayo ya ulaya ni mwendelezo wa sera ya kubadili utawala kama ilivyofanyika kwa Libya.

Urusi na china zimetishia kutumia kura yao ya VETO kwa maazimio yoyote ya kumwekea vikwazo Assad. India na Afrika kusini pia wameungana na Urusi na China katika kupinga mpango huo.