UGIRIKI

Umoja wa ulaya wakubaliana kuipa mkopo nchi ya Ugiriki

Jean-Claude Trichet, presidente del Banco Central Europeo, en Fráncfort el 4 de agosto de 2011.
Jean-Claude Trichet, presidente del Banco Central Europeo, en Fráncfort el 4 de agosto de 2011. © Reuters

Shirika la fedha Duniani IMF pamoja na Umoja wa Ulaya EU hatimaye wamekubaliana kuipatia mkopo mwingine wa fedha nchi ya Ugiriki wenye zaidi ya dola bilioni 11 ikiwa ni awamu ya pili ya mkopo wa awali ulioahidiwa kupatiwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa benki ya umoja wa Ulaya Jean-Claude Trichet ndiye aliyetangaza uamuzi huo hii leo baada ya kumalizika kwa mkutano wa bunge la Umoja wa ulaya na kuonya kuwa endapo nchi wanachama wa umoja huo hawatachukua hatua za haraka kunusuru mataifa yao katika mdororo wa uchumi huenda hali ikawa mbaya zaidi.

Licha ya kutolewa kwa mkopo huo, viongozi hao wameitaka nchi ya ugiriki kuzitumia vizuri fedha hizo na kulipa deni lake kwa wakati kulinga na hali ya uchumi wa taifa hilo utakavyoendelea kuimarika.