LIBYA

Wapiganaji wa baraza la mpito nchini Libya wateka makao makuu ya Polisi mjini Sirte

Mapigano makali yameendelea nchini Libya katika mji wa Sirte kati ya wapiganaji wa baraza la mpito la NTC na wafuasi wanaomuunga mkono kanali Muamar Gaddafi.

Wapiganaji wa Baraza la mpito wakiwa katika mji wa Sirte
Wapiganaji wa Baraza la mpito wakiwa katika mji wa Sirte Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zilizopatikana toka katika mjii huo zinasema kuwa wapiganaji wa waasi wameaafnikiwa kuteka majengo ya makao makuu ya polisi ya Sirte licha ya kuripotiwa upinzani mkali toka kwa wafuasi wa kanali Gaddafi waliosalia kwenye mji huo.

Miji ya Sirte na bani walid ndio miji pekee ambayo imesalia kuwa ngome kubwa ya wafuasi wa kanali Muamar Gaddafi ambao wameendelea kupigana na majeshi ya NTC huku baadhi yao wakiripotiwa kukimbilia mji wa Bani Walid.