MAREKANI-IRAN

Serikali ya Iran yakana kuhusika na njama za mauaji ya balozi wa Saudi Arabia.

Serikali ya Iran imekanusha vikali maofisa wake kushiriki kupanga njama za kufanya shambulio la kigaidi dhidi ya balozi wa Saudi Arabia mjini New York marekani na kuituhumu nchi hiyo kwa kufanya propaganda kuichafua Iran.

Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder akizungumza na waandishi wa habari Washington DC.
Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder akizungumza na waandishi wa habari Washington DC. Win McNamee/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Iran inakuja kufuatia matamshi ya mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Eric Holder kutangaza kuwashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na kupanga njama za kutaka kulipua msafara wa balozi wa saudi arabia nchini humo.

Mwenasheria huyo ameyataja makosa ambayo yanawakabili raia hao kuwa ni pamoja na kushiriki njama za kufanya ugaidi na kukutwa na silaha za milipuko.

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton amesifu juhudi za vyombo vya usalama nchini humo kwa kufanikiwa kuwakamata watu hao na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuitenga nchi ya Iran kutokana na kitendo hiki.