ISRAEL

Vingozi wa kundi la Hamas na Israel wakubaliana kubadilishana wafungwa.

Gilad Shalit, askari jeshi wa Israel anaeshikiliwa na Hamas
Gilad Shalit, askari jeshi wa Israel anaeshikiliwa na Hamas UPJF

Viongozi wa kundi la Hamas na wale wa Israel hatimaye wamekubaliana kubadilishana wafungwa zaidi ya 1000 wakipalestina ili kumwachia mwanajeshi wa Israel aliyetekwa nyara mwaka 2006.

Matangazo ya kibiashara

Ni miaka mitano sasa imetimia toka kutekwa nyara kwa Gilad Shalit mwanajeshi wa Israel aliyetekwa nyara na wapiganaji wa kundi la hamas mwaka 2006 wakishinikiza kuachiliwa kwa wapiganaji wake zaidi ya 1000.

Hatua hiyo inafikiwa baada ya baraza la mawaziri nchini Israel kupitisha mapendekezo ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ya kutaka kuachiliwa huru kwa wafungwa 1000 wakipalestina kwa kubadilishana na Shalit.

Akiongea mara baada ya kikao cha baraza la mawaziri, waziri mkuu Netanyahu amesema kuwa jana usiku aliongea na wazazi wa Shalit na kuwatoa wasiwasi kuhusu mtoto wao na kuwaahidi kutimiza ahadi aliyoitoa awali ya kuhakikisha anamrejesha nyumbani mwanajeshi huyo.

Maelfu ya wananchi wamejitokeza katika ukanda wa gaza kusherekea taarifa hizo huku wakiamini kuwa wataonana na ndugu zao ambao walikuwa wanashikiliwa kwa miongo kadhaa katika magereza ya Israel.