MAREKANI-SAUDI ARABIA-IRAN

Marekani yashinikiza Iran juu ya njama za kumuua balozi wa Saudi Arabia.

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama REUTER S/ Jason Reed

Marekani imeendelea kuongeza shinikizo kwa Iran wakiitaka itoe majibu ambayo yanafaa kutokana na raia wawili kukamatwa wakihusishwa na njama za kutaka kumuua Balozi wa Saudi Arabia wakiwa na uhusiano na taifa hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Barack Obama amesema wataongeza vikwazo zaidi kwa nchi hiyo wakati huu ambapo vyombo vya sheria na usalama vinaendelea na uchunguzi wake kubaini ushiriki wa Iran kwenye tukio hilo.

Rais Obama ameweka bayana hili lililotokea si kati ya Marekani na Iran bali inahusisha nchi ya Saudi Arabia kwa hiyo wanataka uchunguzi ufanyike pamoja na wao kutangaza hatua watakazochukua.

Hayo yanakuja baada ya mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder  kutaja makosa ambayo yanawakabili raia kadhaa wa Iran kuwa ni pamoja na kushiriki njama za kufanya ugaidi na kukutwa na silaha za milipuko.