SYRIA-EU

Watu 19 wapoteza maisha Syria

Wanajeshi wa Syria katika harakati za kupambana na waandamanaji nchini humo.
Wanajeshi wa Syria katika harakati za kupambana na waandamanaji nchini humo.

Majeshi ya Serikali ya Syria yameendelea kukabiliwa na upinzani kutoka kwa waandamanaji nchini humo na taarifa zinaeleza kuwa watu kumi na kenda wamepoteza maisha wakati huu ambapo Umoja wa Ulaya ukitangaza vikwazo vipya.

Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wa Haki za Binadamu nchini Syria wamethibitisha kuuawa kwa watu hao baada ya kutokea kwa mapambano baina ya wananchi na wanajeshi katika Miji ya Banash na Idlib iliyopo Kaskazini Maghabiri mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa serikali ya Rais Bashar Al Assad wanaendelea kuwadhibiti waandamanaji ambao wanataka mabadiliko ya kisiasa hali ambayo imekuwa ikichangia ongezeko la vifo kitu ambacho kinapingwa na wanaharakati.

Hatua hii inakwenda sambamba na vikwazo vipya ambavyo vimetangazwa na Umoja wa Ulaya EU ambao umeamua kushikilia mali za Banki ya Biashara ya Syria zilizopo katika mataifa ya Ulaya.

Mkuu wa Sera za Kimataifa wa Umoja wa Ulaya EU Catherine Ashton wamesema wanaendelea kuweka vikwazo ili kukomesha ukatili ambao unafanywa na Utawala wa Rais Assad dhidi ya wananchi.