Ulaya-Asia

Sarafu ya Euro yaonekana kuimarika barani Asia

Waziri wa uchumi wa Ufaransa Francois Beroin akijadiliana na waziri mkuu wa Luxembourg
Waziri wa uchumi wa Ufaransa Francois Beroin akijadiliana na waziri mkuu wa Luxembourg le progres

Thamani ya Euro katika masoko mengi barani asia imeonekana kuimarika huku wachambuzi wa masuala ya uchumi wakitupia jicho mkutano ujao wa mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya watakaojadili kuhusu kuimarisha sarafu hiyo katika ukanda wao.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya hapo jana umeahidi kwa nchi za 20 zenye utajiri wa viwanda G20 kuhakikisha umoja huo unachukua hatua madhubuti za kukabiliana na mdororo wa kiuchumi kauli inayokuja saa chache baada ya kukamilika kwa mkutano wa mawaziri wa fedha wa G20 mjini Paris Ufaransa.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo waziri wa fedha wa Ufaransa Francois Baroin amesema kuwa umoja wa ulaya utatoa majibu mazuri juma lijalo wakati viongozi wa umoja huo watakapokutana mjini Brussels kujadili hali ya uchumi katika mataifa yao.