Libya-NTC

Baraza la mpito nchini libya NTC lathibitisha kifo cha kanali Muamar Gaddafi

AFP

Baraza la mpito nchini Libya la NTC limethibitisha kifo cha Kiongozi wa zamani wa  Libya Kanali Muamar Gaddafi kilichotokea katika mji alikozaliwa wa Sirte baada ya wanajeshi wa serikali ya mpito kufanikiwa kuchukua uthibiti wa mji huo hivi leo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka kwa viongozi wa serikli ya mpito nchini humo zinaeleza kuwa,Kadhafi aliuawa baada ya msafara aliokuwa anasafiria akitoroka mji huo wa Sirt , kushambuliwa na majeshi ya NATO na baadaye kupigwa risasi na wapiganaji hao.

Ripoti zingine zinaeleza kuwa kanali Gaddafi aliuawa baada ya kupatikana akiwa amejificha ndani ya shimo katika mji huo wa Sirte baada majeshi ya serikali ya mpito kuuchukua.

Mahmoud Jibril Waziri Mkuu wa serikali hiyo ya mpito amenukuliwa akithibitisha kuuawa kwa Kadhafi.

Kwa muda wa miezi minane sasa wapiganaji nchini Libya wakiungwa mkono na majeshi ya NATO wamekuwa wakipigana usiku na mchana kumuangusha Gaddafi, kwa kuiteka miji ya Sirte, Benghazi na Tripoli.

wananchi wa Libya wameonekana kuwa na furaha kwa kifo hicho cha Muamar Gaddafi ambaye ameongoza Libya kwa zaidi ya miaka 40. Wapiganaji hao wanasema kuwa histroria imewekwa na wanaamini kuwa sasa wako huru.

Waziri wa habari katika serikali ya mpito Mahmoud Shammam, aliyethitibisha kufarikiki kwa Gaddafi amesema washirika wengine wa Gaddafi watakamatwa.
Wakati huo, Msemaji wa kanali Muamar Gaddafi,  Mussa Ibrahim yeye anaelezwa kukamatwa na wapiganaji hao.

Aboubakr Younès Jaber aliekuwa waziri wa ulinzi wa kanali Gaddafi ameuawa pia mjini Sirte.