Kenya-Somali

Ndege za kivita za Kenya zaendeleza mashambulzi nchini Somalia

Ndege zas Kivita za Kenya zimeendelea kufanya mashambulizi nchini Somalia kulenga ngome za Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab ambao wanaaminika ndiyo wanaowateka watalii akiwemo raia wa Ufaransa aliyefariki jana Marie Dedieu.

Wanajeshi wa Kenya wakipanda lori kwenye mpaka wa Kenya na Somalia
Wanajeshi wa Kenya wakipanda lori kwenye mpaka wa Kenya na Somalia STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kenya ambayo imeanzisha operesheni inayokwenda kwa jina la Linda Nchi Dhidi ya Al Shabab imejiapiza kuhakikisha inawasaka kila sehemu ambayo wanamgambo wa Al Shabab wamejificha.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula naye ameendelea na msimamo wake kuwa hawajaivamia Somalia lakini wanachokifanya ni kutoa msaada kwa majirani zao.

Operesheni hiyo ya Kenya imekosolewa vikali na wachambuzi wa mambo kwamba Kenya isingelitekeleza operesheni hiyo, bali ingelijiunga na jeshi la AU liloko Somalia ambalo linapambana na Al Shabab tangu kitambo.