Umoja wa Ulaya

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kujadili hali ya uchumi katika ukanda huo

Guetty Images/ Emrah Turudu

Viongozi wa Ulaya wanatarajiwa kujadilia hali ya uchumi katika Ukanda huo wakati huu ambapo maandamano yamechacha katika nchi kadhaa yakipinga hatua za serikali zao kutaka mpango wa ubanaji wa matumizi kwa lengo la kukuza uchumi.  

Matangazo ya kibiashara

Ugiriki, Ujerumani na Uhispani ni nchi ambazo zimeshuhudia maandamano ikiwa ni muendelezo wa hali ya sintofahamu ambayo inaukumba uchumi wa mataifa kadhaa barani Ulaya kwa sasa.

Ugiriki yenyewe imeshuhudia makabiliano makali baina ya waandamanaji ambao wameitisha mgomo wa saa arobaini na nane kupinga mpango wa kubana matumizi ambao umepigiwa kura na bunge nchi humo hiyo jana.

Wafanyakazi wa umma wanapinga vikali hatua zinazopendekeza na serikali ambazo ni pamoja na kupunguza wafanyakazi pamoja na kuongeza kodi ili iweze kulipa deni ambalo nchi hiyo inadaiwa na Umoja wa Ulaya EU.

Bunge nchini Ugiriki baada ya kupiga kura yake hiyo jana wanatarajiwa kurejea tena na kupiga kura kwa mara nyingine hapo kesho huku Mji wa Athen ukishuhudia wananchi wakipambana na askari.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anatarajiwa kukutana na Kansela wa Ujerumani Angela merkel kujalidi mgomo wa kiuchumi unaoendelea pamoja na kusaka mbinu za kuisadia Ugiriki.