Syria

Risala yenye ujumbe mzito kwa rais wa Syria Bashar Al Assad kutoka jumuia ya nchi za kiarabu

Jumuia ya nchi za kiarabu imemtumia risala yenye ujumbe mzito rais wa Syria Bashar Al Assad yakumdhirishia uchungu walionao viongozi wa jumuia hiyo kuhusu mauaji ya raia yanayoendelea nchini Syria. Vyombo vya usalama vimewafyatulia risase hapo jana watuwaliokuwa wakiandamana na kuwauawa watu arobaini. Mawaziri wa jumuia ya nchi za kiarabu wanataraji kukutana na kiongozi wa Syria katika mkutano unatarajiwa kufanyika kesho jijini Doha nchini Quatar.

Reuters/Handout
Matangazo ya kibiashara

Ni mara ya kwanza Juimuia ya nchi za kiarabu inapaza sauti kukemea hali inayoendelea nchini Syria tangu pale yalipoanza machafuko, mbali na ujumbe wa mawaziri wa Umoja wa nchi za Kiarabu uliozuru nchini humo octoba 26 iliopita.

Ujumbe huo uliwasilisha pendekezo la kuanzisha mazungumzo baina ya serikali ya Damascus na upinzani kwenye makao makuu ya juimuia hiyo jijini Kairo.Serikali ya Damascus ilionyesha nia ya kuzungumza na upinzani, lakini kutekeleza nia hiyo imekuwa kitendawili.

Wanaharakati waliandamana jana wakiunga mkono Syria iwekewe vikwazo vya anga. Jeshi la nchi hiyo liliwasambaratisha na kuwauawa watu arobaini katika purukushani hizo.