Australia

Mamia ya wasafiri wakwama nchini Australia baada ya shirika la ndege la Qantas kusitisha safari zake ndani na nje ya nchi.

Shirika la ndege la Qantas limesimamisha huduma za safari za ndege nchini Australia, na nje ya taifa hilo kwa muda usiojulikana, kutokana na tatizo la kiviwanda. Hatua hiyo imesababisha mamia ya wasafiri kukwama katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini humo, na hatua ya kusitisha safari hizo inaelezwa kuwa ya kushtukiza.

Ndege za shirika la Qantas nchini Australia
Ndege za shirika la Qantas nchini Australia Reuters/Fred Prouser
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Autsralia Julia Gillard anaonya kuwa hatua hiyo huenda ikisababisha kushuka kwa uchumi wa taifa hilo ikiwa suluhu la haraka halitapatikana. Wafanyakazi wa shirkika hilo la ndege wamekuwa mara kwa mara wakijihusisha na migomo ya mara kwa mara, na hivyo kusabisha shirika hilo la Qantas kupata hasara ya Dola Millioni 16 kila wiki.

Uhusiano kati ya shirika la ndege la Qantas na vyama vya kutetea maslahi ya wafanyikazi wa shirika hilo la ndege nchini humo ulidorora kuanzia mwezi wa nane mwaka huu, baada ya shirika hilo kutangaza kuwa lilikuwa na mipango ya kuanzisha huduma zake barani Asia.
 

Wafanyikazi wa shirika hilo wanataka maslahi zaidi ikiwa ni pamoja na kuongezewa mishahara na kuhakikishiwa usalama kazini, kutokana na kupanda kwa maisha.
 

Shirika la Qantas linamiliki asimilia 65 ya safari zote za ndege za ndani nchini Australia.