Libya-NTC

Abdel Rahim Al Keib achaguliwa kuwa waziri mkuu wa Libya

Waziri mkuu mpya wa Libya Abdel Rahim Al Keib akipongezwa na kiongozi wa baraza la NTC
Waziri mkuu mpya wa Libya Abdel Rahim Al Keib akipongezwa na kiongozi wa baraza la NTC REUTERS/Ismail Zetouny

Utawala wa Muda nchini Libya hatimaye umechagua Waziri Mkuu mpya mtaalam wa teknolojia na mfanyabiashara Abdel Rahim Al Keib kwa ajili ya kuongoza mchakato wa kuijenga upya nchi hiyo chini ya Baraza la Taifa la Mpito NTC.

Matangazo ya kibiashara

Al Keib amechaguliwa baada ya kupigwa kura za wazi na wanachama wa NTC na kufanikiwa kupata kura ishirini na sita kati ya hamsini na moja zilizopigwa na Kiongozi wake Mustafa Abdel Jalil amesema kura hiyo ni ishara ya ujenzi upya wa taifa hilo.

Al Keib dakika kadhaa baada ya kukabidhiwa jukumu la kuwa Waziri Mkuu wa Libya chini ya Utawala wa NTC hakusita kuainisha kibarua ambacho atakabiliwa nacho kuijenga nchi hiyo.

Kuchaguliwa kwa Waziri Mkuu huyu mpya kunakuja wakati Opresheni ya Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO ikimalizaka.

Libya kwa sasa itakabiliwa na jukumu la kuhakikisha inajenga demokrasia ya kqweli katika taifa hilo sambamba na kurejeaha utulivu katika nchi hiyo iliyoshuhudia miezi tisa ya mapambano yaliyouangushwa Utawala wa Marehemu Kanali Muammar Gaddafi.