Marekani-Palestina

Marekani yafuta msaada wake kwa UNESCO

Wajumbe wanachama wa shirika la UNESCO
Wajumbe wanachama wa shirika la UNESCO Reuters/B.Tessier

Serikali ya Marekani imefutilia mbali msaada wake wa dola milioni sitini kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi ya Utamaduni UNESCO kutokana na kuunga mkono hatua ya Mamlaka ya Palestina kupatiwa uanachama wa Umoja wa Mataifa UN.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO walipiga kura jana jijini Paris Ufaransa ya kupasisha Palestina kuwa mwanachama wa shirika hilo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland ametangaza uamuzi huo wa kuutiliambali msaada huo kwa kile ambacho kinaonekana UNESCO kwenda kinyume na Marekani ambayo kupitia Rais Barack Obama ilisema itatumia turufu yake kupinga hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al Maliki amepongeza hatua ambayo imefikiwa na UNESCO ya kuwaunga mkono na kusema hili ni jambo la kihistoria kwani nchi yake inahitaji haki yake.