UGIRIKI-ATHENS

Baraza la mawaziri nchini Ugiriki labariki kuitishwa kwa kura ya maoni kuamua hatma ya nchi hiyo kwenye Umoja wa Ulaya

Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou
Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou REUTERS/Thierry Roge

Baraza la Mawaziri nchini Ugiriki kwa pamoja limeunga mkono mpango wa Waziri Mkuu wa Taifa hilo George Papandreou wa kuitisha kura ya maoni kuamua juu ya kuchukuliwa kwa mkopo kutoka Umoja wa Ulaya EU au la.

Matangazo ya kibiashara

Papandreau aliuambia mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kuwa hatua ya kufanyika kwa kura ya maoni ni muhimu sana ili kufikia uamuzi wa kutekelezwa kwa mpango wa kubana matumizi hatua iliyoamriwa nchi wanachama wanaotumia sarafu ya Euro.

Katika mkutano uliomalizika usiku wa jana Papandreau amewaambia mawaziri kuwa serikali inahitaji ridhaa ya raia wa ugiriki ili kufikiwa kwa lengo hilo.

Serikali ya ugiriki inakabiliwa na kura za wabunge juu ya kuwa na imani na sera ya Papandreau ama la,kura zitakazopigwa siku ya ijumaa.

Papandreau anatarajiwa kukutana na viongozi wa ulaya nchini ufaransa hii leo,kabla ya kufanyika mkutano wa Mataifa 20 tajiri duniani,mkutano utakaofantika mjini Paris Ufaransa.