NIGERIA-DAMATURU

153 wauawa nchini Nigeria katika shambulio la bomu

Ramani ya maeneo mashambulizi yalipotokea
Ramani ya maeneo mashambulizi yalipotokea Reuters

Takriban watu 150 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi ya risasi na mabomu kaskazini mwa Nigeria ambapo kundi la kiislam lenye msimamo mkali Boko Haram hapo jana lilikiri kuhusika na mashambulio hayo.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo limesema kuwa limehusika katika mashambulizi ya jimbo la Borno na Damaturu na kwamba litaendelea kushambulia serikali mpaka pale vikosi vya usalama vitakapoacha kuwashtaki wafuasi wake.

Rais wa Nigeria,Goodluck Jonathan amekemea vikali mashambulizi hayo huku maafisa wakisema kuwa polisi wanafanya uchunguzi kubaini wahusika wa mashambulio hayo.

Shambulio la ijumaa la mabomu na risasi lililenga vituo vya polisi,kambi za jeshi na makanisa katika miji ya Damaturu,Maiduguri na miji mingine miwili midogo.

Mashambulizo hayo yamekuja baada ya mashambulio matatu ya kujitoa Muhanga yalipotekelezwa dhidi ya makao makuu ya jeshi mjini Maiduguri na jimbo la Borno.