IRAN

Iran yasema mataifa ya magharibi hayana uthibitisho kuwa inampango wa kutengeneza silaha za Nuklia

waziri wa mambo ya nje wa Iran Ali Akbar Salehi
waziri wa mambo ya nje wa Iran Ali Akbar Salehi Reuters/Esam Al-Fetori

Iran imesema hii leo kuwa nchi za magharibi hazina ushahidi kuwa inatengeneza silaha za Nuklia, kauli ilityotolewa wakati huu ambapo taarifa ya shirika la atomiki la kimataifa IAEA likitarajia kutoa ushahidi mpya dhidi ya Tehran.

Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika ziara katika nchi jirani ya Armenia, Waziri wa mambo ya nje Ali Akbar Salehi amesema hakuna uthibitisho kuwa Iran itatatengeneza silaha za Nuklia.

Salehi amesema kuwa Marekani na mataifa ya magharibi zinaweka mashinikizo bila ushahidi na hoja za msingi dhidi ya Iran.

Ripoti ya shirika la IAEA inatarajiwa kutolewa wiki hii ,huku wanadiplomasia wakisema kuwa ripoti hiyo italenga juu ya taarifa kuhusu jitihada za makusudi za Iran za kutengeneza madini ya uranium na silaha.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad hapo jana aliishutumu Israel na Marekani kwa hatua yao ya kutafuta kuungwa mkono kuishambulia kijeshi nchi yake akieleza kuwa hatua hilo ni kosa kubwa sana.