ITALIA

Berlusconi kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu

Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi
Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi Reuters/Alessandro Bianchi

Waziri mkuu wa Italia silvio, Berlusconi amesema hatagombea tena wadhifa wa uwaziri mkuu na kwamba atajiuzulu ikiwa Mswada wa kufanya mabadiliko ya Bajeti utapitishwa na Bunge la nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Berlusconi amesema atajiuzulu mwishoni mwa mwezi huu, wakati huu ambapo chama cha Berlusconi kikitaka kufanyika kwa uchaguzi mpya huku upinzani ukitaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa .

Bunge la Italia linatarajiwa kupitisha mabadiliko ya bajeti mwishoni mwa mwezi huu ili kunusuru uchumi wa nchi hiyo ulioanza kuyumba ikiwa ni athari ya mzigo wa madeni ulioikumba ulaya.

Wakati huohuo jopo kutoka umoja wa ulaya unatarajiwa kuwepo mjini Roma nchini humo ili kufuatilia kwa karibu ni namna gani Italia inapanga namna ya kupambana na mzigo wa madeni.

Kamishna wa maswala ya fedha ndani ya umoja wa ulaya, Olli Rehn amesema atawasilisha matokeo ya utafiti huo mwishoni mwa mwezi huu, huku akikiri kuwa hali ya kiuchumi nchini Italia inatia wasiwasi.