LIBERIA-MONROVIA

Kura za duru la pili la uchaguzi nchini Liberia zahesabiwa

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea Reuters/Luc Gnago

Kura za duru la pili la uchaguzi nchini Liberia zinahesabiwa hii leo huku rais wa nchi hiyo na mshindi wa Tuzo la amani la Nobel Ellen Johnson Sirleaf akitumainiwa kuwa Mshindi.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ulikuwa ukitarajiwa kuwa wa amani na kuthibitisha kuimarika kwa demokrasia,lakini kugoma kwa mpinzani wa Sirleaf,Winston Tubman na vurumai zilizosababisha takriban watu wanne kupoteza maisha,kumeleta hali tete ya kisiasa nchini humo.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa kesho huku tayari Tubman ameweka wazi kuwa hatayatambua matokeo hayo baada ya kudai kuwa Matokeo ya duru la kwanza yalijaa udanganyifu na upendeleo kwa Sirleaf.

Tubman amedai kuwa alipangiwa njama za kuuawa katika tukio la ufyatuaji risasi kutawanya maandamano siku ya jumatatu,huku polisi ikikana madai hayo na kuyaita ya kipuuzi.

Kura za jana zilipigwa kwa amani,huku kukiwa na watu wachache waliojitokeza ikiwa ni asilimia 72 ya waliojiandikisha kupiga kura.