UGIRIKI

Mchakato wa uundwaji wa serikali ya umoja nchini Ugiriki kutangazwa hii leo

waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreau
waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreau Reuters/Costas Baltas

Mchakato wa uundwaji wa serikali ya Mpito ya ugiriki utatangazwa baadae hii leo, Tangazo lililokuja wakati ambapo mazungumzo yakiendelea kwa siku ya tatu sasa.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreau aliyeridhia kuondoka madarakani, atakuwa na mazungumzo na viongozi wa vyama mbalimbali nchini humo baada ya kukutana na rais.

Mazungumzo yamekuwa yakiendelea kati ya Papandreau na kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani cha New Democracy, Antonis Samara, mazungumzo yaliyoanza siku ya jumatatu.

Bado haijawekwa wazi ikiwa kuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa baada ya mazungumzo ya hapo jana huku kukiwa na taarifa kuwa viongozi hao hawajaamua bado ni nani atakayeongoza serikali ya umoja.

Taarifa zinasema kuwa Samaras hajaridhishwa na matakwa ya nchi za ukanda unaotumia sarafu ya Euro, Eurozone na mashirika ya fedha.