IRAN

Ufaransa yatishia kuweka vikwazo dhidi ya Iran

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad
Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad Reuters路透社

Ufaransa imetoa wito wa kuwekwa kwa vikwazo dhidi ya Iran, ikiwa nchi hiyo itaendelea na kukaidi wito wa jumuia ya kimataifa wa kuacha mpango wa urutubishaji wa Nuklia baada ya shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki, IAEA kusema kuwa Tehran imekuwa ikiendeleza teknolojia ya utengenezaji wa silaha za Nishati hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema kuwa ikiwa Iran itakataa kufuata matakwa ya jumuia ya kimataifa na kukaidi kutoa ushirikiano,wako tayari kuweka vikwazo vikali dhidi yake.

Wizara hiyo imedai kuwa ripoti ya IAEA imeeleza kuwa shughuli zinazofanywa na na Iran zinakiuka maazimio ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na baraza la kimataifa la nguvu za Atomiki.

Taarifa za IAEA zinasema uwepo wa shughuli za kijeshi na urutubishaji wa madini ya Uranium kwa wingi nchini Iran kunatoa picha yenye mashaka juu ya dhamira ya Iran.

Mashaka yaliyopo hivi sasa ni kuwa Iran ina lengo la kutengeneza mabomu ya Nuklia chini ya Mwamvuli wa madai kuwa mpango wa urutubishaji wa Uranium ni kwa ajili ya matumizi Chanya.

Katika hatua nyingine, Makamu mkuu wa vikosi vya kijeshi vya Iran ametoa onyo hii leo kuwa shambulio lolote dhidi ya Iran litaleta uharibifu mkubwa nchini humo na kwamba vitisho hivyo vitaathiri pia maeneo yaliyo nje ya Mashariki ya kati.