SYRIA

Watu wanne wauawa na vikosi vya usalama vya nchini Syria

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad (REUTERS)

Raia wanne nchini Syria wameuawa baada ya Vikosi vya usalama nchini humo kuwafyatulia risasi waandamanaji nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo la ushambuliaji wa Raia limefanyika mjini Damascus huku taarifa kutoka kwa wanaharakati wa haki za binaadam nchini humo zikisema kuwa raia watatu akiwemo mtoto mmoja waliuawa huku kumi wengine walijeruhiwa.

Mji uliozungukwa na vikosi vya kijeshi vya Syria vimeendesha msako , mahojiano na operesheni ya kamatakamata katika harakati ya kuwakamata wanamgambo wanaopinga utawala wa rais wa nchi hiyo Bashar Al Assad.

Wanaharakati wa haki za binaadam wamesema kuwa jana pekee watu 20 wakiwemo wanajeshi wanane na raia 12 waliuawa mjini Homs.

Hayo yamejiri baada ya wiki iliyopita rais Assad alitia saini mapendekezo ya mpango wa kutafuta amani na kumaliza machafuko,na kuachwa huru kwa wafungwa waliokamatwa kwa makosa ya kufanya maandamano halikadhalika makubaliano juu ya kuondoa vikosi katika miji mbalimbali nchini humo.