IRAN

Iran yaapa kujibu Mashambulizi dhidi ya nchi itakayo jaribu kuivamia

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Ayatollah Ali Kamenei
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Ayatollah Ali Kamenei Reuters/Leader.ir/Handout

Iran imesema itajibu shinikizo lolote ,mashambulizi na tishio lolote la kijeshi litakalotolewa dhidi yake, kauli ambayo imekuja baada ya Israel kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya Tehran vya kutengeneza silaha za Nuklia.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa mapinduzi ya Kiislam chini Iran, Ayatollah Ali Khamenei amewaambia wanafunzi katika chuo cha kijeshi mjini Tehran kuwa ujumbe huo unakwenda kwa maadui wote wa Iran hasa America, Israel na washirika wake.

Kauli ya kiongozi huyo wa kidini imekuja baada ya kuwepo kwa vitisho wiki iliyopita kutoka kwa rais wa Israel, Shimon Perez kuwa kuna uwezekano wa kutekelezwa kwa mashambulizi ya anga dhidi ya mitambo ya Nuklia ya Iran.

Iran, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikikana mpango wa kurutubisha  Nuklia kwa sababu za kijeshi, imesema haitakaa kimya na kushuhudia vitisho kutoka mataifa ya Magharibi.

Ingawa haikuelezwa hatua zitakazochukuliwa na Israel,taarifa za vyombo vya habari wiki iliyopita zimesema kuwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi, Ehud Barak wanatafuta kuungwa mkono na baraza la Mawaziri juu ya mpango wa kuishambulia Iran.

Iran imesema nchi yeyote itakayojaribu kulivamia taifa hilo ni lazima ijiandae kupata upinzani wenye nguvu kutoka Iran.