UTURUKI

Vikosi vya uokoaji vyaendelea kuwatafuta manusura wa ajali ya tetemeko la ardhi nchini Uturuki

Ramani ya Uturuki
Ramani ya Uturuki

vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kutafuta watu waliokwama kwenye vifusi baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi la kipimo cha ritcha cha 5.6 huko mashariki ya uturuki tetemeko lililosababisha takriban watu saba kupoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Majengo 25 yameanguka ikiwemo hoteli ya ghorofa sita mjini Van,huku kukiwa na taarifa kuwa watu 23 wameokolewa wakiwa hai na takriban 100 wakiwa hawajulikani walipo.

Mwezi uliopita tetemeko la ukubwa wa 7.2 kipimo cha ritcha kilipiga eneo hilohilo na kusababisha watu 600 kupoteza maisha.

Mamlaka nchini Uturuki imeshutumiwa vikali juu ya namna ilivyoshughulikia tetemeko lililotokea mwezi uliopita.