LIBERIA-MONROVIA

Mpinzani Winston Tubman kushirikiana na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kuijenga Liberia.

Mpinzani nchini Liberia Winston Tubman
Mpinzani nchini Liberia Winston Tubman

Mpinzani aliyesusia uchaguzi wa Liberia,Winston Tubman leo hii ameridhia kufanya kazi pamoja na rais wa nchi hiyo Ellen Johnson Sirleaf baada ya kuwepo kwa vuguvugu la kisiasa lililotishia mgawanyiko katika taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika amethibitishwa rasmi kuwa mshindi wa matokeo ya kura za duru la pili la uchaguzi baada ya Tubman kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho na kuwataka wafuasi wake wasusie uchaguzi huo.

Tubman amesema kuwa ingawa Sirleaf hivi sasa anadai kuwa Rais wa Liberia na anatambuliwa na jumuiaya ya kimataifa, ni lazima watafute namna ya kushirikiana nae.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Liberia ilitangaza kuwa kura zilihesabiwa kutoka asilimia 86.6 ya vituo vya uchaguzi, huku Sirleaf akishinda kwa asilimia 90.8 huku Tubman akipata asilimia 9.

Katika hatua ningine, Sirleaf ameahidi kuunda tume huru kufanya uchunguzi juu ya shambulio la risasi la jumatatu, baada ya askari wa usalama kukiri kuwafyatulia risasi waandamanaji.