MAREKANI-IRAN

Marekani yatoa wito kwa Iran juu ya mpango wa nyuklia

waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani  Hillary Clinton
waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton BA

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema Marekani inafanya mashauriano na washirika wake na ametoa wito kwa serikali ya Iran juu ya kushughulikia maswala ya hivi karibuni kuhusu mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia.

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na ongezeko la mvutano kati ya nchi ya iran na maadui zake wawili wakuu, Israel na Marekani baada ya taarifa ya Umoja wa Mataifa kutolewa kuwa ushahidi unaonyesha mpango wa Iran juu ya tafiti zake hususan katika matumizi ya nyuklia.

Iran ambayo muda wote imekuwa ikikanusha madai hayo yote katika mpango wake wa nyuklia imejibu hatua hiyo na kusema haihofii taarifa iliyotolewa na shirika la  Umoja wa Mataifa  la nguvu za nyuklia, na kuongeza kuwa ipo tayari kukabiliana na shambulio lolote.

Nchi ya Iran imekuwa ikikanusha tuhuma kwamba inaunda zana za kinyuklia nakusema kuwa inarutubisha madini ya uranium kwa uzalishaji wa kawaida kwa matumizi yake na kwa manufaa ya wananchi wake.

Kwa matokeo ya ripoti hiyo Marekani sasa inapendekeza kuwa nchi hiyo iwekewe vikwazo zaidi kutokana na ripoti yake inaashiria kwamba utafiti wa kisayansi unaofanyika nchini Iran unaonyesha kuwa ina mipango ya kijeshi.