UFARANSA-NIGERIA

Serikali ya Ufaransa kushirikiana na Nigeria katika vita dhidi ya Ugaidi

Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa na mweziwe wa Nigeria Henry Odein
Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa na mweziwe wa Nigeria Henry Odein France diplomatie

Serikali ya Ufaransa imeahidi kushirikiana na nchi ya Nigeria katika kupambana na matukio ya ugaidi ambayo yameishambulia nchi hiyo siku za hivi karibuni na kusababisha vifo vya mamia ya raia nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Alain Juppe amesema hayo akiwa nchini Nigeria katika ziara yake yenye lengo la kufanya mazungumzo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili juu ya kupambana na ugaidi hususan baada ya taifa hilo la Afrika magharibi kukumbwa na ishara za mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni.

Waziri huyo ameelezea kusikitishwa na mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Boko Haram katika maeneo ya Damaturu na Maiduguri nchini humo na kuahidi kujiandaa kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi katika taifa hilo.

Sambamba na hayo kiongozi huyo anatarajiwa kuhudhuria kutiwa saini ya mpango wa fedha zenye thamani ya dola za Marekani milioni moja kwa ajili ya mradi wa shirika la maendeleo la Ufaransa wenye lengo la kuboresha usafiri wa umma katika mji mkuu wa Lagos.