DAMASCUS-SYRIA

Umoja wa nchi za Kiarabu watishia kuifuta uanachama Syria

Raia wa Syria wakiandamana nje ya jengo la makao makuu ya Umoja wa nchi za Kiarabu mjini Cairo, Misri
Raia wa Syria wakiandamana nje ya jengo la makao makuu ya Umoja wa nchi za Kiarabu mjini Cairo, Misri Reuters

Maelfu ya wananchi wa Syria wameandamana katika maeneo mbalimbali ya nchini humo, kuonesha kuchukizwa kwao na hatua ya Umoja wa nchi za Kiarabu kutishia kuifuta uanachama katika Umoja huo kutokana na kushindwa kuzua machafuko yanayoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa rais Bashar al-Asad waliandamana nje ya ofisi za ubalozi wa Saudi Arabia nchini humi wakiituhumu nchi hiyo kwa kuunga mkono maazimio ambayo yamefikiwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Cairo, Misri.

Viongozi wa Umoja huo wametoa siku tatu kwa nchi ya Syria kuhakikisha inamaliza machafuko nchini mwake ama sivyo kukabiliwa na adhabu ya kufutiwa uanachama.

Yussef Ahmad ambaye ni balozi wa Syria katika Umoja huo ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ambayo imefikiwa na mawaziri wa nchi wanachama na kukikata kitendo hicho kuwa kimeenda kinyume na katiba ya Umoja huo.

Ahmad ameongeza kuwa kitendo ambacho Umoja huo unataka kukifanya kinakwenda kinyume na niwazi kuwa vongozi wake wameanza kuongozwa na propaganda za mataifa ya magharibi kama walivyofanya kwa nchi ya Libya.