Marekani

Marekani kuimarisha uhusiano wa kijeshi na Australia

Reuters/Jason Reed

Rais wa Marekani, Barack Obama yuko ziarani nchini Australia kuhusu mambo ya kidiplomasia ambapo amesema kuwa nchi yake itaimarisha uhusiano wa kijeshi na Australia.Ziara hiyo ya siku mbili ya Rais Obama inalenga kuimarisha uhusianao wa kiusalama wa miaka zaidi ya 60 baina ya pande hizo mbili na inakuwa ni ziara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Marekani mwaka 2008.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuwasili nchini humo hii leo, Obama amelakiwa na mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Australia Julian Gillard kabla ya kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa kiusalama ambapo nchi hizo zimekubaliana kuuimarisha zaidi.

Rais Obama anatarajiwa kulihutubia bunge la nchi Australia kabla ya kuondoka kuelekea katika mji Darwin ulioko kaskazini mwa nchi hiyo ambako anatarajiwa ataainisha mpango wa ushirikiano katika jeshi la majini ikiwemo mafunzo ya kijeshi.

Makubaliano hayo ya ushirikiano wa kijeshi hayatamaanisha kuwa Marekani itakuwa na kambi ya kudumu nchini Australia lakini maafisa wa Serikali ya Obama huo ni mpango kuimarisha zaidi uwepo wa Majeshi ya Marekani.

Rais Obama amesema kuwa katika kuimarisha uhusiano huo wa kijeshi Marekani itapeleka Australia wanajeshi wa majini wasiopungua 250 na wanatarajiwa kuwasili huko mwaka ujao.