Myanmar

Suu Kyi atangaza kurejea katika siasa nchini Myanmar, Arroyo akamatwa Ufilipino

REUTERS/Soe Zeya Tun

Kinara wa Siasa na Mpinzani Mkuu wa Siasa nchini Myanmar Aung San Suu Kyi ametangaza hatua yake ya kurejea kwenye ulingo wa siasa wakati huu ambapo marekani imetangaza kumpeleka Waziri wake wa mambo ya Nje nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Suu Kyi ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ametoa kauli hiyo wakati huu ambapo nchi yake ikisubiri ujio wa kwanza wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani katika kipindi cha miaka hamsini.

Rais Barack Hussein Obama amesema wakati umefika wa kufanyika mabadiliko ya kisiasa nchini Myanmar baada ya muda mrefu kushudia utawala wa kijeshi ukikandamiza demokrasia.

Wakati huohuo Rais wa zamani wa Ufilipino Gloria Arroyo amekamatwa katika Hospital ya Manila kama ambavyo Mahakama iliagiza kufuatia mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake kwa kuhusika kwenye ulaghani katika uchaguzi.

Msimamizi Mwandamizi wa Polisi James Bucayo amethibitisha kukamatwa kwa Arroyo na kwa sasa yupo chini ya ulinzi katika Kituo Cha Polisi kilichopo Kusini mwa nchi hiyo kabla hajafikishwa mahakamani.

Arroyo ambaye alipata kibali cha Mahakama Kuu nchini Ufilipo kwenda nchini Singapore kupatiwa matibabu amekwama kuondoka baada ya kuwekewa vizuizi na serikali inayoongozwa na Rais Benigno Aquino.