Umoja wa ulaya

Mataifa ya ulaya yakubaliana kubana matumizi

Reuters/François Lenoir

Serikali za mataifa 27 ya umoja wa ulaya pamoja na bunge la ulaya, zimekubaliana kupunguza matumizi ya Euro bilioni 129 katika bajeti ya mwaka 2012 sawa na asilimia mbili zaidi ya bajeti ya mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Naibu waziri wa fedha Jacek Dominic ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika hapo jana hadi majira ya usiku, amesema kuwa makubalianao hayo yamefikiwa bila kupingwa.

Kamishina wa bajeti ya ulaya Janusz Lewandowski ameelezea makubaliano hayo kama hatua ya kubana matumizi kufuatia kuwepo kwa mzigo wa madeni unaozuia nchi za jumuiya Ulaya kuwa na matumizi makubwa.

Uchumi wa umoja wa ulaya umeendelea kutetereka kufuatia nchi wanachama kukabiliwa na mzigo wa madeni jambo lililopelekea kuwepo maazimio ya mpango wa kubana matumizi ili kunusuru uchumi wa umoja huo.