LIBYA

Mtoto wa Gaddafi,Seif Islam akamatwa kusini mwa Libya

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya,kanali Gaddafi,Seif Al Islam
Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya,kanali Gaddafi,Seif Al Islam

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya kanali Moamer Gadafi,Seif al Islam amekamatwa katika eneo la kusini mwa libya akiwa na wasaidizi wake 2 wakiwa katika harakati za kutorokea nchini Niger.

Matangazo ya kibiashara

Afisa mwandamizi wa baraza la taifa la mpito nchini Libya bashir al twahyiib amethibitishia vyombo vya habari ambapo waziri wa sheria Mohammed al-Allagui amesema seif al islamu amekuwa akitafutwa ili kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Kufuatia kukamatwa kwa Seif Al Islam,waziri wa sheria Mohammed Al-Allagui amesema  taarifa zaidi itatolewa juu ya uamuzi uliofikiwa baada ya muda mfupi. 

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ilitoa vibali mwezi juni 27 dhidi ya seif al islam sambamba na baba yake kutokana na mashtaka ya kukiuka haki za binadamu wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ya kanali gadafi.