UINGEREZA-SYRIA

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza kukutana na waasi wa Syria jumatatu

AFP / ALEXANDER JOE

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague anatarajia kufanya mazungumzo na kiongozi wa waasi nchini Syria siku ya jumatatu katika jiji la London ambapo pia atakutana na wanachama wa upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Tarifa kutoka kwa msemaji wa ofisi ya mambo ya nje nchini Uingereza inaeleza kuwa waziri Hague atakutana na wawakilishi kutoka baraza la taifa la Syria pamoja na kamati ya taifa ya uratibu wa mabadiliko ya demokrasia baada ya miezi kadhaa ya mawasiliano ya nyuma ya pazia.

Chanzo cha habari nchini Syria kimesema kuwa Damascus ingekubali waangalizi wa utekelezaji wa mpango wa amani lakini kwa masharti maalum.

Ghasia zimekuwa zikiendelea nchini Syria wakati tarehe ya kukomeshwa kwa ghasia hizo iliyowekwa na umoja wa mataifa ya kiarabu ikikaribia ikiitaka serikali hiyo kukomesha vitendo vya ukandamizaji juu ya waandamanaji ambapo siku ya jumatano Syria ilisimamishwa rasmi na umoja wa kiarabu.