UHISPANIA

Raia nchini Uhispania wajitokeza kupiga kura.

REUTERS.

Raia nchini Uhispania wameripotiwa kujitokeza kwa wingi kuelekea katika vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kuleta mabadiliko kwa serikali iliyopo katika kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Katika uchaguzi huo mgombea wa chama kinachoongoza serikali cha Sosholisti ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Alfredo Perez Rubalcaba anakabiliwa na upinzani mkali toka kwa mpinzani wake Mariano Rajoy Brey wa chama cha Mlengo wa kati cha Popula.

Kura za maoni zilikipa ushindi chama cha mlengo wa kati kinachoongozwa na Mariano Rajoy Brey dhidi ya chama cha kisosholisti kinachoongoza serikali jambo ambalo linaashiria ushindi kwa chama cha Mariano Rajoy.

Uchaguzi huo umeitishwa na waziri mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero kufuatia matatizo ya kiuchumi kulikumba taifa hilo ingawa yeye mwenyewe hagombei katika uchaguzi huo.