LIBYA

Seif al Islam kufikishwa mahakama ya ICC.

Msemaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita Fadi el-Abdallah amesema kuwa nchi ya Libya inao wajibu wa kisheria kumfikisha Seif al-Islam mahakamani ili uamuzi wa mwisho juu ya Kesi inayomkabili ufikiwe na majaji.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imekuja muda mfupi baada ya afisa mwandamizi wa jeshi la baraza la mpito nchini libya Bashir Al Twayib kuthibitisha kukamatwa kwa mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa libya kanali Muamarr Gaddafi, Seif al Islam Gaddafi.

Miongoni mwa kesi zinazo mkabili Seif al Islam ni pamoja na kushiriki vitendo vya kikatili na kufanya mauaji ikiwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu pamoja na kuratibu mashambulizi dhidi ya raia yaliyofanywa na vikosi vya usalama enzi za utawala wa Gaddafi.