CAIRO-MISRI

Wananchi wa Misri waendelea kusalia katika uwanja wa Tahrir

Waandamanji wakikabilina na Polisi jirani na uwanja wa Tahrir
Waandamanji wakikabilina na Polisi jirani na uwanja wa Tahrir Reuters/Ahmed Jadallah

Mapambano kati ya polisi na waandamanaji yameendelea kushika kasi nchini Misri kushinikiza kung'oka madarakani kwa Utawala wa Kijeshi chini ya Field Marshal Mohamed Hussein Tantawi ikiwa yameingia siku ya saba hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wameendelea kutunishiana misuli na polisi ambao wanatumia mabomu ya machozi, risasi za mpira na vifaru kuwasambaratisha waandamanaji ambao wanaonekana kula kiapo cha kutaka utawala wa kiraia kwa sasa.

Mashambulizi makali yameshuhudiwa katika majiji ya Cairo na Alexandria ambapo waandamanaji wameanza kupata nguvu baada ya wanajeshi kuasi na kuamua kuungana na wananchi wakisema wanataka kuwalinda na ukatili unaofanywa dhidi yao.

Viunga vya Tahrir vimeshuhudia maelfu ya wananchi wakiendelea kupiga kambi huku wakichangizwa na nyimbo ambzo zinashinikiza kuondoka madarakani kwa Utawala wa Tantawi.

Tangu kuzuka kwa maandamano hayo mapya yanayoshinikiza uwepo wa serikali ya kiraia nchini Misri watu thelathini na watano wamepoteza maisha huku wengine elfu tatu na mia mbili hamsini wakijeruhiwa.