TRINIDAD-TOBAGO

Waziri mkuu wa Trinidad na Tobago, Kamla Persad-Bissessar anusurika kuuawa

Waziri mkuu wa Trinidad and Tobago, Kamla Persad-Bissessar
Waziri mkuu wa Trinidad and Tobago, Kamla Persad-Bissessar Reuters

Vyombo vya Usalama nchini Trinidad na Tobago vinawashikilia watu kumi na wawili kwa kutekeleza shambulizi lililoshindwa la kutaka kumuua Waziri Mkuu Kamla Persad-Bissessar pamoja na mawaziri wengine wa serikali.

Matangazo ya kibiashara

Kamishna wa Polisi Dwayne Gibbs amethibitishwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumi na wawili baada ya kufanyika msako uliowajumuisha wanajeshi na polisi wapatao mia moja na kubahatika kuwakamata hadi walinzi wa jadi.

Waziri Mkuu Persad-Bissessar amesema jaribio hilo la kumuua limeshindwa kutokana na mafanikio ya sheria ya hali ya hatari ambayo imewekwa katika nchi hito tangu tarehe ishirini na moja mwezi August.

Katika hotuba yake kwa wananchi waziri mkuu Persad-Bissessar amewashutumu baadhi ya viongozi wa Serikali yake kwa kushiriki katika njama ya kumuua akihusisha tukio la hatua yake ambayo aliitangaza mwezi wa nane mwaka huu kusaka makundi ya kijambazi nchini humo.

Waziri mkuu huyo pia aliituhumu Serikali ya Marekani kwa kuyafadhili baadhi ya makundi nchini humo na kudai kuwa Serikali yake inaushahidi kuonesha maofisa wake wa usalama kushirikiana na baadhi ya makundi nchini humo.

Kufuatia shambulio hilo ulinzi umeendelea kuimarishwa nchini humo hasa kwa maofisa wa juu wa serikali kuhofia kutokea kwa shambulio jingine kama hilo ambapo linaelezwa kuwa ni la kwanza kuwahi kufanywa nchini humo kulenga viongozi wa juu wa serikali.