IRAQ

Watu 15 wauwawa katika shambulio la mabomu nchini Iraq.

Mmoja wa majeruhi wa bomu akiwa hospitalini  mjini Baghdad nchini Iraq.
Mmoja wa majeruhi wa bomu akiwa hospitalini mjini Baghdad nchini Iraq. AFP

Watu kumi na watano wamefariki dunia na wengine ishirini na wanane wamejeruhiwa katika matukio tofauti ya shambulio la mabomu yaliyotokea hii leo katikati mwa mji wa Iraq maofisa wa usalama nchini humo wamethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Katika shambulio la kwanza mabomu yamelipuka katika pande mbili za barabara itokayo Abu Ghraib Magharibi mwa mji wa Baghdad kuelekea Fallujah na kupiga gari ambalo lilikuwa limebeba wafanyakazi wa ujenzi.

Maofisa wameongeza kuwa katika tukio la pili mabomu matatu yamelipuka katika eneo la Baab al- Sharqi na kuua watu saba na kujeruhi wengine ishirini na wanane.

Jumla ya waliopoteza maisha katika matukio yote mawili ni watu kumi na watano huku majeruhi wakifikia idadi ya watu ishirini na wanane.