MISRI

Chama cha kiislamu cha Muslim Brotherhood chataka kuunda serikali baada ya uchaguzi wa wabunge

Waandamanaji katika bustani ya Tahrir jijini Cairo nchini Misri
Waandamanaji katika bustani ya Tahrir jijini Cairo nchini Misri ©Reuters.

Wanaharakati nchini Misri wanaendelea kupiga kambi katika bustani ya Tahriri jijini Cairo,kushinikiza kujizulu kwa baraza la kijeshi nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao wanasema kuwa wamechoka na uongozi huo wa kijeshi na hakuna jipya ambalo wameliona katika uongozi wao tangu,kupinduliwa kwa serikali iliyopita.

Wakati mapambano hayo yakiendelea,uchaguzi wa wabunge nchini humo untarajiwa kufanyika Jumatatu hii,uchaguzi ambao ni wa kwanza tangu kupinduliwa kwa rais zamani wa taifa hilo Hosni Mubarak.

Wachambuzi wa kisiasa nchini humo wanasema chama cha kiislamu cha Muslim Brotherhood kinatarajiwa kuibuka na ushindi,kwa sababu kina nafasi kubwa ya kufanya hivyo kutokana na umaarufu wake wa kuuangusha utawala wa Mubarak.

Uongozi wa chama cha Muslim Brotherhood umesema ,baada ya uchaguzi huo unastahili kupewa jukumu la kuunda serikali kama raia wanavyotaka.

Hata hivyo, uongozi wa kijeshi kupitia kiongozi wake Mohammed Hussein Tantawi  umesema kuwa uchaguzi wa urais utafanyika mwaka ujao mwezi Juni .