Syria

Mawaziri wa muungano wa nchi za kiarabu wapitisha vikwazo dhidi ya Syria

Mawaziri wa fedha wa nchi za kiarabu wakiwa Cairo Misri
Mawaziri wa fedha wa nchi za kiarabu wakiwa Cairo Misri (REUTERS)

Mawaziri wa fedha kutoka muungano wa nchi za kiarabu wamepitisha vikwazo dhidi ya serikali ya Syria, inayoongozwa na rais Bashar Al-Asaad,kutokana na mauji yanayoendelea dhidi ya waandamanaji,pamoja na kukataa wangalizi kutoka kwa muungano huo kuchunguza mauji hayo.

Matangazo ya kibiashara

Kati ya mataifa 22 ya muungano huo 19 yameunga mkono vikwazo hivyo,huku Iraq na Lebanon zikiepuka kushiriki katika zoezi hilo.
 

Miongoni mwa vikwazo hivyo vilivyopitishwa ni pamoja na kuwazuia viongozi wa serikali ya rais Asaad kuzuru taifa lolote la kiarabu pamoja na kustaafisha mali ya serikali iliyowekezwa katika mataifa mbalimbali ya muungano huo.
 

Kikwazo kingine ni pamoja na kusitisha kwa safari za ndege kutoka Syria kwenda katika mataifa ya kiarabu pamoja na kusitisha huduma zozote na benki kuu ya Syria,pamoja na kusitisha miradi yeyote ya maendeleo kutoka kwa muungano huo nchini Syria.
 

Wanajeshi wa serikali nchini Syria,wamewaua raia kumi katika mji wa Homs,katika shinikizo zinazoendelezwa na waandamanaji nchini humo kumtaka rais Bashar Al Asaad kujiuzulu.
 

Kikwazo kingine ni pamoja na kusitisha kwa safari za ndege kutoka Syria kwenda katika mataifa ya kiarabu pamoja na kusitisha huduma zozote na benki kuu ya Syria,pamoja na kusitisha miradi yeyote ya maendeleo kutoka kwa muungano huo nchini Syria.
 

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu elfu 3 wameuawa mikononi mwa wanajeshi wa Syria tangu maandamano dhidi ya rais Bashar Al Asaad yalipoanza mapema mwaka huu.