DRCongo-Uchaguzi

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwapokea wataalamu wa maswala ya uchaguzi kutoka Marekani

Wataalamu wa maswala ya uchaguzi kutoka Marekani
Wataalamu wa maswala ya uchaguzi kutoka Marekani

Ujumbe maalumu wa wataalamu wa masuala ya kura toka nchini Marekani wanatarajiwa kuwasili nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC mnamo mwezi ujao kwa lengo la kuishauri tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uhesabiaji kura za wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Juma hili tume ya taifa ya uchanguzi nchini DRC CENI ilitangaza kuahirisha zoezi la uhesabiaji wa kura za wabunge mpaka pale wataalamu toka nchini Marekani na Uingereza watakapowasili kwa ajili ya kusaidia zoezi hilo.

Hatua ya kutaka msaada wa wataalamu toka nchini Marekani inakuja kufuatia ukosolewaji mkubwa wa uchaguzi wa Urais ambao unadaiwa kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi wakati wa uhesabiaji wa kura hizo na hivyo kutotaka tatizo hilo kujirudia wakati wa uhesabiaji wa kura za wabunge.

Zaidi ya wagombea elfu 19 walisimama kugombea nafasi ya ubunge ambapo wote kwa pamoja wanawania nafasi 500 za bunge la nchi hiyo.