Umoja wa Mataifa UN

Licha ya bajeti ya Umoja wa Mataifa UN Kupunguzwa, katibu mkuu wa UN anaimani kuwa watafaanikiwa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon RFI

Licha ya wajumbe wa baraza la Umoja wa mataifa kupitisha na kupunguza bajeti ya Umoja huo kwa asilimia tano, katibu mkuu Ban Ki Moon ameendelea kusisitiza kuwa licha ya bajeti ndogo iliyopitishwa lakini anaimani itafanya kazi kwa yale ambayo yamepangwa kufanywa ndani ya miaka miwili ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Umoja wa mataifa wamepunguza kwa asilimia tano bajeti ya umoja huo ambapo sasa utatumia kiasi cha dola bilioni 5.15 ukilinganisha na bajeti ya miaka miwili iliyopita ambayo ilikuwa ni dola bilioni 5.41 na hivyo kuifanya kuwa bajeti ndogo zaidi kupitishwa na umoja huo.

Ban Ki Moon mbali na kupongeza wajumbe wa umoja huo kwa kufanya maamuzi hayo pia amepongeza kazi ambayo imefanywa na umoja huo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.